Wednesday, July 09, 2014

KATIBA:Silaa asisitiza serikali mbili ni lazima

Siku moja baada ya kuelezwa kuwa msimamo wa kung’ang’ania serikali mbili ni maagizo ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Jerry Silaa amesisitiza kuwa serikali mbili ni lazima.

Silaa, ambaye pia ni Meya wa Ilala jijini Dar es Salaam, alitoa kauli hiyo juzi kwenye hafla ya kuwasimika makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM mkoani Mbeya.

‘’Wananchi wa Mbeya, kwa niaba ya Kamati Kuu ya CCM, nasema muundo wa muungano kwenye Katiba Mpya ni Serikali mbi… mbili, mbi... mbili, mbi.. mbili,” alisema Silaa.

Juzi gazeti hili lilimkariri Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi akifungua Baraza la UVCCM wa Mkoa wa Mbeya, akisema kuwa msimamo huo ni maagizo ya Rais Kikwete.

Mbali ya kauli hiyo ya Silaa, vijana wa CCM waliohudhuria hafla hiyo walivaa fulana za kijani zilizoandikwa nyuma “2 Zinatosha”. “Namshukuru (kamanda wa hamasa wa Chipukizi wa CCM) Paul Makonda kwa ufafanuzi alioutoa kuhusu sababu za CCM kukataa mfumo wa serikali tatu, kwamba unalenga kutoa nafasi ya wanasiasa wengi zaidi kupata madaraka na hivyo kusababisha hasara kwa wananchi,” alisema.

Awali, Makonda alisema malengo makuu ya kuandika Katiba Mpya ni yale yanayogusa maisha ya Watanzania wengi badala ya wanasiasa wachache.

“Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iseme wazi jinsi ya kuongeza ajira kwa vijana, iseme wazi jinsi ya kuondoa ufisadi nchini; iseme wazi haki ya kupata matibabu; itoe haki kwa wanawake; wazee iwatetee wanyonge ili wafaidike na rasilimali za Taifa,” alisema Makonda.

Alisema yeye akiwa mmoja wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba anawashangaa wanasiasa wachache ambao wameamua kushupalia suala la muundo wa Muungano ambao kimsingi hauna manufaa kwa Watanzania wengi.

“Manufaa ya serikali tatu ni makubwa kwa wanasiasa kupata vyeo, lakini pamoja na CCM kujua hilo inaona utakuwa mzigo kwa Watanzania,” alisema. BONYEZA HAPA HUONE 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment