Wednesday, July 09, 2014

Chuji ndo bhaasi tena Azam fc

BIASHARA ya Azam FC kumsajili kiungo mkongwe Athuman Idd ‘Chuji’ imekufa rasmi baada ya nyota huyo kuambiwa hakuna kitakachoweza kufanyika tena kwani wasiomtaka wameshinda vita.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata na kuthibitishwa na uongozi wa Azam ni kwamba hakuna uwezekano wa kumsajili tatizo kubwa likielezwa kuwa ni rekodi zake za utovu wa nidhamu ambazo zimewagawa viongozi.

“Uongozi umesitisha usajili wa Chuji, amefanya mazoezi kwa siku moja tu baada ya hapo siku ya pili hakuja mwenyewe lakini baadaye uongozi ukawasiliana naye na kumwambia zoezi la kusajili limesitishwa rasmi, unajua mengi yamezungumzwa likiwemo la kuweza kutuvuruga kwa nidhamu yake ndogo,” alisema bosi huyo.

Katibu Mkuu wa Azam Nassoro Idrisa ‘Father’ alikiri kusitishwa kwa Chuji akisema: “Nikweli hilo lipo uongozi wetu tumekubaliana kuwa hatutaweza kumsajili tena, tulikuwa tunahitaji kipaji chake lakini suala la nidhamu ndiyo lililowapa mashaka viongozi wenzangu kwa hiyo hatatakuwa naye tena.” BONYEZA HAPA HUONE 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment