KIUNGO wa Azam FC, Frank Domayo amerudi rasmi nchini akitokea Afrika Kusini alikofanyiwa upasuaji lakini akazuiwa kurudi kwao na kufichwa katika chumba maalumu kwa wiki sita.
Domayo aliyerudi nchini juzi Jumamosi kwa Ndege ya South African Airways kwa sasa mguu wake hautagusa sakafu wala ardhi badala yake atakuwa kule Chamazi yalipo mabweni ya timu hiyo akitakiwa kuwa katika utulivu wa hali ya juu kwa muda huo, kwa mujibu wa ratiba aliyopewa na daktari aliyemfanyia upasuaji huo Rob Nicholas.
Akizungumza na Mwanaspoti daktari mkongwe wa tiba za michezo nchini Mwanandi Mwankemwa amesema upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa na moja ya sharti alilopewa Domayo ni kutakiwa kuwa katika utulivu wa hali ya juu na kuhakikisha analikamilisha hilo nyota huyo ataishi kwa wiki sita katika mabweni hayo ya Azam.
“Atakuwa hapa Chamazi kwenye chumba maalumu tulichomwandalia, hatakuwa peke yake atakuwa na Joseph Kimwaga ambaye naye anatakiwa kutulia kama Domayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
“Akiwa pale atapata kila kitu anachotaka, hatutaki kumrudisha kwao kwa sababu lolote linaweza kutokea akaweza kuupa msukosuko huu mguu ambao anatakiwa kutouchezesha kwa wiki sita.” Akizungumzia upasuaji huo Domayo alisema; “Kwa kweli kama unavyoniona naumwa lakini ninafuraha kutokana na kulimaliza hili tatizo nilikuwa sijui litamalizika lini kila nilipokuwa nauangalia ule uvimbe, nawashukuru Azam sidhani kama nitawasahau kirahisi kwa hili walilonifanyia.” BONYEZA HAPA HUONE
UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon







0 comments:
Post a Comment