Tuesday, July 08, 2014

Fabregas afichua kila kitu kuhusu chelsea

KIUNGO Cesc Fabregas amesema hakushawishiwa na mtu kuhusu kujiunga na Chelsea na huo uliokuwa uamuzi wake binafsi.

Staa huyo Mhispaniola ameihama Barcelona na kutua Chelsea katika uhamisho unaotajwa kuigharimu klabu hiyo ya Stamford Bridge pauni 27 milioni.

“Hapana, haukuwa uamuzi wao hata kidogo, wamekuwa nikiwaambia kwamba watanikumbuka sana. Rais alijaribu kunizuia, lakini nilimweka wazi kuhusu mipango yangu, akanielewa,” alisema Fabregas, ambaye juzi alishuhudia kikosi chake cha Hispania kikifungasha virago mapema na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko nchini Brazil.

“Nilizungumza na Andoni Zubizarreta (mkurugenzi wa michezo) na Josep Bartomeu (Rais wa Barca) na kuwaeleza kwamba nataka kuondoka. ukweli ni kwamba kila kitu kilikuwa chepesi sana. Nimeamua na naamini katika uamuzi wangu. “Kama ningedhani sitakwenda kuwa na furaha Chelsea, basi nisingefanya uamuzi huu mkubwa kabisa katika maisha yangu.

Najua nitakuwa na furaha tu, kwa sababu niliishi London kwa miaka minane, nina marafiki wengi. Nitakuwa na familia yangu na ni umbali wa saa moja na nusu tu kutoka Barcelona.” Kuhusu uamuzi wa kuihama Barcelona na kama Lionel Messi alimshawishi abaki, Fabregas alisema: “Si kweli kinachosemwa kwamba klabu ilimtuma Messi. Leo hajawahi kuniambia nibaki. Kama unatufahamu vizuri, utajua tu hawezi kufanya kitu kama hicho.

Leo ni mtu wa kweli, aliniambia atakuwa na furaha kwa chochote nitakachofanya.” BONYEZA HAPA HUONE 


UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon

0 comments:

Post a Comment