| BROM, SESSEGNON 'ALIYETIWA
MFUKONI' TAIFA AWATIA KIMOJA, SARE
2-2
BAO la dakika ya 87 la kiungo Daley Blind
limeinusuru Manchester United kulala mbele
ya West Brom Albion baada ya kupata sare
ya 2-2 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu
England usiku huu.
Blind alifunga bao zuri kutoka umbali wa
mita 23, likiwa bao lake la kwanza tangu
ajiunge na Mashetani hao Wekundu msimu
huu.
Stephane Sessegnon aliyeshindwa
kufurukuta mbele ya Tanzania, Taifa Stars
akiichezea Benin ikifungwa 4-1 katika
mchezo wa kirafiki Oktoba 12 Uwanja wa
Taifa mjini Dar es Salaam, leo aliifungia
WBA bao la kwanza dakika ya nane
akimalizia krosi ya Andre Wisdom.
Marouane Fellaini aliyetokea benchi dakika
ya 46 kuchukua nafasi ya Ander Herrera,
aliisawazishia Manchester United dakika ya
48 akimalizia pasi ya Angel di Maria.
Mzaliwa wa Burundi, Saido Berahino
akaifungia bao lililoelekea kuwa la ushindia
West Brom dakika ya 66 akimalizia pasi ya
Chris Brunt, kabla ya Blind ‘kuchomoa’
dakika za lala salama.
Kikosi cha Manchester United kilikuwa: De
Gea, Rafael, Jones, Rojo, Shaw, Blind,
Herrera/Fellaini dk46, Januzaj, Mata/Falcao
dk72, Di Maria/Ashley Young dk76, Van
Persie
West Brom: Myhill, Wisdom, Lescott,
Dawson, Pocognoli, Gardner, Brunt, Morrison,
Dorrans, Sessegnon/Youssuf Mulumbu dk86
na Berahino. |
0 comments:
Post a Comment