Sunday, September 21, 2014
 |
| Mpenzi msomaji wa safu hii ya Exclussive
Interview baada ya kumaliza kusoma
historia ya maisha ya msanii wa filamu
Bongo, Wastara Juma, leo tunakuletea
msan i i mkongwe kwenye tasnia ya filamu
Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.Thea
amefunguka mengi kuhusiana na maisha
yake ya sanaa, karibu uinjoi
mahojiano:Msanii mkongwe kwenye tasnia
ya filamu Bongo, Salome Urassa‘Thea’.
HISTORIA KWA UFUPI
Nimezaliwa mwaka 1982 mkoani
Shinyanga, nimepata elimu ya msingi
katika Shule ya Msingi Igunda iliyopo
Kahama ambapo nilisoma mpaka darasa la
tatu na baada ya hapo nilihamia Shule ya
Msingi Mapambano-Sinza, jijini Dar na
kufanikiwa kuhitimu darasa la saba.
SEKONDARI
Baada ya kuhitimu nilijiunga na kidato cha
kwanza katika Shule ya Sekondari Zanaki
ambako nilisoma kwa mwaka mmoja tu na
kuhamia Sekondari ya Gorio ambako nako
nilisoma kwa mwaka mmoja nikahamia
Kijitonyama ambako nilimalizia kidato cha
tatu na cha nne.
APATA UJAUZITO
Baada ya kuhitimu k i dato cha nne
niliendelea kusoma masomo ya Pre Form
Five lakini ndoto zangu zilikwamia hapo
baada ya kupata ujauzito.
BAHATI MBAYA
Ilitokea bahati mbaya tu na sikuona
sababu ya kutoa mimba ndiyo nikaamua
kuzaa na nikapata mtoto wa kiume
ambaye kwa sasa baba yake alimchukua
anasoma Dubai. Mimba hiyo niliipata
mwaka 2003 nikiwa najiandaa na masomo
ya kuingia kidato cha tano, nilipata
ujauzito na kuamua kuzaa ambapo nilipata
mtoto wa kiume anayejulikana kwa jina la
Maron Bimpela.
HAWAKUWA NA MALENGO YA NDOA
Sisi hatukuwa na malengo ya kuoana bali
nilipopata ujauzito na kujifungua baba
mtoto ali endelea kumtunza mtoto mpaka
alipokuwa mkubwa akaja kumchukua,
ndoto zangu za kusoma ziliishia hapo.
RASMI KWENYE SANAA
Baada ya kujifungua sikuendelea tena na
masomo bali niliendelea na sanaa kwani
tangu nikiwa kidato cha nne nilikuwa
nafanya sanaa hivyo niliingia rasmi.
AKUTANA NA CHIKI
Kwa mara ya kwanza kabisa Chiki Mchoma
ndiye aliyenichukua akanipeleka kwenye
kundi lililokuwa linajulikana kwa jina la
Tunda.
MCHEZO WAKE WA KWANZA
Mchezo wa kwanza kushiriki na kurushwa
Runingani uliitwa Ulimwengu wa Vi jana
ukweli siku hiyo sikulala kutokana na
furaha niliyokuwa nayo. Kwenye kundi hilo
nilidumu kwa muda mfupi sana, kama
miezi tu.
AJIUNGA NA MAMBO HAYO
Baada ya hapo nilijiunga na Kundi la
Mambo Hayo baadaye Kaole na hapo
mpaka sasa naendelea kucheza filamu
ambapo nina filamu za kwangu mwenyewe
sita na nyingine zaidi ya 40 za
kushirikishwa.
UHUSIANO NA BABA MTOTO
Baada ya kujifungua sikuendelea na
uhusiano na baba mtoto wangu. Uhusiano
uliokuwepo ni kwamba alikuwa akimlea
mwanaye tu na baada ya kukua ndipo
akamchukua.
AACHANA NA WANAUME
Baada ya kupata mtoto wangu nilitulia na
kumlea na sikuwahi kujihusisha kimapenzi
na mwanaume yeyote.Nilikaa miaka mingi
sana mpaka nilipokuja kukutana na
Michael Sangu ‘Mike’, tukafunga ndoa.
WALIVYOKUTANA
Mimi na Mike tulikuwa kwenye kundi moja
ambapo nilikuwa namuita kaka na yeye
ananiita mdogo wake lakini alikuwaga
ananitania kwamba lazima atanioa nikawa
naitikia kiutani tu.
Yaani sikuwa hata na wazo la kuolewa na
msanii na nilikuwa nimeshaapa kwamba
sitaolewa na msanii sijui ni kitu gani
kilitokea maana Mike nilikuwa n i memzoea
namuita kaka tukawa tunapiga stori sana
lakini kila wakati alikuwa akiniambia
atanioa nikawa namjibu sawa. |
0 comments:
Post a Comment