AZAM FC haijaweka wazi kuwa imeinunua Klabu ya Moro United lakini uchunguzi wa JOMBITZ umebainisha matajiri hao wameichukua klabu hiyo iliyoshuka daraja.
Moro United ambayo imewahi kutamba Ligi Kuu kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la kwanza ngazi ya mkoa.
Mmoja wa vigogo wa Azam aliliambia JOMBITZ kuwa wameinunua Moro ambayo wataitumia kwa ajili ya kuboreshea wachezaji wao vijana.
Azam inataka kutumia staili ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inavyoitumia Don Bosco kutengeneza na kuboresha viwango vya wachezaji wao.
Uongozi wa Azam umegoma kufafanua suala hilo kwa madai kwamba bado kuna mambo ya kiofisi wanayakamilisha.
Kama bado ujalike ukurasa wetu wa facebook ili kila habari za kimichezo zinaponifikia uzipate kirahisi BONYEZA HAPA
UKIONA TUKIO LOLOTE USISITE KUTUTUMIA PICHA WHATSAPP NO:06570352125 Festo saimon







0 comments:
Post a Comment