Ombi jipya: Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa William Carvalho.
ASERNAL wametuma maombi ya kutaka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, William Carvalho mwenye thamani ya paundi milioni 35.
Washika bunduki wapo katika harakati za kutaka kusajili kiungo wa Ulinzi na wanaiwinda saini ya kinda huyo mwenye miaka 22.
Ingawa inafahamika kuwa Sporting wanahitaji ofa ya paundi milioni 35.6 ili kuvunja mkataba wake.Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, aliichezea timu yake ya taifa kwa dakika 90 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil.
kwa muda mrefu sasa amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United na sasa Asernal wameingia vitani.







0 comments:
Post a Comment