Tuesday, July 01, 2014

SOKA:DIEGO COSTA ATUA RASMI CHELSEA

Chelsea wamethibitisha kumsajili rasmi Diego Costa baada ya kufikia makubaliano na Atletico Madrid.

Chelsea ilitaka kukamilisha usajili huo kabla ya Kombe la Dunia kwa pauni milioni 32. Jambo hilo halikufanikiwa lakini sasa mkataba umefikiwa.

Taarifa iliyotolewa imesema: "Chelsea inathibitisha kufikia makubaliano na Atletico Madrid kwa ajili ya uhamisho wa Diego Costa". Chelsea walikuwa wamekubali kulipa ada ya uhamisho na Diego Costa mwenyewe aliwaambia Atletico hamu yake ya kuondoka, lakini mkataba ulikuwa mgumu kufikiwa.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu  BONYEZA HAPA 


by festo saimon phone 0657035125

0 comments:

Post a Comment