Wednesday, July 02, 2014

Dully sykes kumsimamia Chidbenz

Msanii mkongwe wa muziki na mtayarishaji wa muziki nchini, Dully Sykes amedai kuwa ameamua kumchukua msanii wa Hip Hop Chidi Benz ili afanye naye kazi, ambapo amedai kuwa hawezi kumuacha apotee.  

Akizungumza na jombitz Dully Sykes amesema ameamua kumchukua ili akiweza amrudishe upya. “Mimi Chidi nipo naye kama mdogo wangu tu na tunasaidiana na tunabebana kwasababu mimi siwezi kukubali mtu kama Chidi Benz amedrop halafu mimi nikakaa nikamwangalia halafu studio ninayo, siwezi kukubali, yule ni mdogo wangu namchukulia ni mdogo wangu kabisa, nimetoka naye mbali,” amesema.

“Kwahiyo siwezi nikakubali aendelee kuwa hivi. Nitamtoa mpaka afike katika kilele, arudi katika nafasi yake, hata kama atakuwa na ubaya kwa watu mimi kwangu mimi hajawahi nifanyia ubaya, kwanini nisimchukuwe? Simchukui kama label,” alisema.  BONYEZA HAPA HUONE 


by festo saimon phone 0657035125

0 comments:

Post a Comment