Kuondoka kwa DNA katika label ya Grand Pa Records kulizua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa Afrika mashariki walizoea uwakilishi wake katika familia hiyo kwa muda mrefu.
Msanii huyo alisafisha anga kwa kueleza sababu zilizopelekea yeye kuondoka katika label hiyo kuwa ni uamuzi binafsi unaotokana na mipango yake binafsi ya baadae. “Ni kama business tu yoyote, kwa sababu nimeshatimiza yaani niko huru nifanye renew au niendelee kivyangu”.
DNA aliiambia Power Jams ya East Africa Radio. “So ni uamuzi wangu kwa sababu nimeangalia mambo mengi, yaani mambo yangu ya kibinafsi na future plans nikaona niendelee tu man solo.” Msanii huyo alisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati yake na mmiliki wa label hiyo kama baadhi ya watu walivyodai , na kwamba hii inaweza kuthibishwa kwa tukio la yeye kuwa best man kwenye harusi ya mmiliki wa Grand Pa Records, Refigah wiki kadhaa zilizopita.
Naye mmiliki wa Grand Pa Records alitoa tamko rasmi jana na kueleza kuwa DNA alijitoa Grand Records baada ya pande zote mbili kukubaliana bila kuwepo ugomvi wowote kati yao, na kwamba mahusiano yao bado ni mazuri. Aliongeza kuwa ingawa DNA ameshatoka kwenye label hiyo, wataendelea kuachia nyimbo ambazo alifanya akiwa chini ya label hiyo na kukanusha taarifa kuwa label hiyo ilikuwa na mambo mengi (too busy) kiasi cha kumsahau DNA. “He still have unreleased songs at our stable which will be released according to arrangement between the label and him. We at Grand Pa Records, artists, producer, and staff wish Dennis Waweru Kagia aka DNA all The best in his endevours, God bless the work of his hands.” Ni sehemu ya tamko la Grand Pa. BONYEZA HAPA HUONE
by festo saimon phone 0657035125
by festo saimon phone 0657035125
0 comments:
Post a Comment